
Mazao yaliyosahaulika na yasiyopewa kipaumbele
#Imarisha afya yako kwa kula vyakula bora vitokanavyo na mazao yaliyosahaulika na yasiyopewa kipaumbele yazalishwayo kiikolojia.
Tuyatambue mazao yaliyosahaulika na yasiyopewa kipaumbele
Tuyatambue mazao yaliyosahaulika na yasiyopewa kipaumbele
Mazao yaliyosahaulika na yasiyopewa kipaumbele (NUS) ni mazao yenye viini lishe vingi, lakini kwa namna moja au nyingine yameaachwa/kuupuuzwa kwa sababu ya uelewa hafifu wa umuhimu wake, viinilishe vilivyomo, faida za kiafya (umuhimu wa viinilishe) na matumizi yake hasa katika milo ya kila siku katika kaya au migahawani. Pia ukosefu wa soko ni na mnyororo imara wa thamani ni sababu nyingine ya mazao haya kupuuzwa/kusahaulika.

Mazao yaliyosahaulika na yasiyopewa kipaumbele katika mradi wa CROPS4HD
Mazao yaliyosahaulika na yasiyopewa kipaumbele katika mradi wa CROPS4HD
Kupitia mradi wa (CRPS4HD), SWISSAID inahimiza kilimo cha mazao yenye viinilishe vingi na umuhimu mkubwa kiafya ambayo yamesahaulika/kupuuzwa . Mradi unalenga katika kuboresha uhifadhi wa mbegu kupitia benki za mbegu za jamii, kuongeza upatikanaji wa mbegu za ndani, na kusaidia wakulima wadogo katika kuzalisha mazao hayo. Mbinu hii inalenga kuimarisha usalama wa chakula, lishe, mapato na uendelevu wa mazingira.


Mazao 12 nchini Tanzania
Mazao 12 nchini Tanzania
NJUGU MAWE

Maelezo zaidi

ULEZI

Maelezo zaidi

MCHICHA (Majani)

Maelezo zaidi

MCHICHA (Mbegu)

Maelezo zaidi

MABOGA



Maelezo zaidi

BOGA

MBEGU ZA MABOGA

MAJANI YA MABOGA

NYANYA CHUNGU

Maelezo zaidi

MNAVU

Maelezo zaidi

MGAGANI

Maelezo zaidi

UFUTA

Maelezo zaidi

BUNGO

Maelezo zaidi

TOPETOPE

Maelezo zaidi

MATEMBELE

Maelzo zaidi

Bidhaa za NUS zilizotengenezwa Tanzania
Bidhaa za NUS zilizotengenezwa Tanzania
Aina za Vyakula/Mapishi Yatokanayo na mazao ya NUS
Aina za vyakula/mapishi yatokanayo na mazao ya NUS
Mangungu
Njugu mawe na mahindi yaliyokobolewa,
Chemsha mahindi kisha weka njugu mawe,ongeza mafuta/tui la nazi/karanga/mbegu za maboga/ufuta na endelea kupika mpaka kiive,ongeza chumvi kidogo na chakula kipo tayari kwa kuliwaMaboresho: Ili kuongeza viini lishe katika chakula hiki, inashauriwa kuongeza mbogamboga za kijani dakika 5 kabla ya kuepua chakula

Chipwenje (Mseto)
Njugu mawe,mtama uliokobolewa/mchele
Chemsha njugu mawe mpaka ziive kisha weka mchele/ mtama uliokobolewa,mafuta na chumvi koroga na wacha viive kwa pamoja. Maboresho: Chakula hiki ni vizuri kiliwe na mboga za majani na matunda kama bungo,topetope, chungwa n.k au juisi za matunda halisi.

Futari zenye mboga mboga
Maboga,njugu mawe, mchicha(mboga inayopatikana), tui la nazi
Chemsha njugu mawe kiasi cha kuiva, weka maboga chemsha, weka mboga mboga na nazi wacha jikoni kwa dakika 5 kisha unaweka chumvi unakoroga na futari inakua tayari

Maandazi ya maboga
Unga wa ngano 700gm,maboga 300gm,sukari na chumvi 5gm na mafuta ya mimea 1000mls
Chemsha boga wacha lipoe. Ponda ponda boga changanya na ngano,hamira,sukari,chapa mandazi,chumvi na ladha upendayo kutengeneza donge kwa kutumia maji uliyochemshia boga. Acha iumuke kisha kata vipande na kaangaa kwenye mafuta.

Chapati za maboga
Maboga 200gm, unga wa ngano 800gm, sukari 50gm, chumvi 50gm na mafuta 200mls
Chemsha boga acha lipoe. Ponda ponda na changanya na unga wa ngano na ladha uipendayo, kanda kwa kutumia maji uliyochemshia boga kama yatakuwa yamebaki kutengeneza donge, kata vipande,sukuma kisha kaanga

Uji
Unga (Njugu mawe,Ulezi,mchele, na mbegu za maboga), nazi,ubuyu,sukari na chumvi
Chemsha maji, pembeni koroga unga kwenye maji ya baridi kicha mimina kwenye maji yaliyochemka huku unakoroga kuepuka kutengeneza mabonge, acha uji uchemke mpaka uive. Weka tui la nazi na sukari/chumvi uache uchemke kwa muda usiozidi dakika 5. ongeza ubuyu epua, uji wako uko tayari.

Ugali wa Njugu mawe (njugu 50% na Mahindi 50%)
Unga wa njugu mawe uliochanganywa na mahindi, maji
Chemsha maji, pembeni koroga unga kwenye maji ya baridi kicha mimina kwenye maji yaliyochemka huku unakoroga, acha uji uchemke kisha ongeza unga na endelea kukoraga hadi ugali utakavyokuwa mzito kulingana na uzito upendao, acha kwa dakika mbli uive, epua na ugali wako upo tayari. Ugali huu unaweza kuliwa na mboga mbali mbali ikiwemo nyama/maini, moga za majani dagaa nk.

Ugali wa Maboga
Boga (ukubwa kulingana na mahitaji) unga wa mahindi,ngano isiykobolewa, mtama nk
Andaa boga lako kisha pika hadi liive viizuri
ponda ponda hadi lilaainike kama ujiuji ( unaweza kuongeza maji kidogo kama boga halina maji mengi)
ongeza unga upendao na endelea kusonga kama ugali hadi utakapoona umepata uzito upendao.
Acha jikoni kwa mida wa dakika mbili hivi ili uive vizuri.
Ipua na ugali wako upo tayar.
Ugali huu unaweza kuliwa na dagaa, nyama, mboga za majani na hata samli.

Saladi ya Njugu mawe
Njugu mawe zilizopikwa
Kitunguu 1
Nyanya 1
Parachich 1
Ndizi mbivu 1
Mafuta ya mimea kama alizeti, nazi, mafuta ya mchikichi
Chambua, pepeta, osha njugu mawe kisha pika hadi ziive vizuri
Chambua, osha kisha Katakata matunda na mboga mboga ukubwa upendao
Chukua bakuli na kisha changanya njugu matunda na mboga mboga na changanya vizuri.
Weka mafuta kiasi kidigo ili kuongeza Ladha,mvuto,muonekano na hasa viinishe kwenye saladi.
Note. Hii inaweza kutumika kama mlo na pia huweza kuliwa na pilau, chipsi , ndizi za kukaanga nk

Tembele
Matembele fungu 1
Karoti 1
Nyanya 1 ( sio lazima)
Mafuta ya mimea 10mls
Chumvi
Chambua matembele na osha vizuuri
Kata kata upendavyo ( sio lazima kukata waweza kupika bila kukaka )
Weka sufuria jikoni na weka mafuta.
Mafuta yakipata moto weka kitunguu na kanga mpaka kiive kisha weka karoti na endelea kukaanga.
Weka matembele yako na funika kisha pika kwa moto mdogo kwa muda wa dakika mbili hadi tatu.
Geuza na ongeza chumvi kisha funika ten ana pika kwa dakika mbili au tatu.
Matembele yapo tayari ipua na mbpga hii ni tamu sana ikiliwa na ugali, wali, pilau, ndizi nk

Mchicha
Majani ya mchicha fungu 1
Kitunguu kidogo 1
Mafuta ya kupikia 10mls
Chambua osha na kisha kata kata mchicha wako vipande upendavyo
Kata kata kitunguu
Weka sufuria/kikaango jikoni na acha kikauke.
Ongeza mafuta na kisha kanga kitunguu hadi kiive. ( unaweza kuongeza mboga mboga zingine upendavyo)
Weka mchicha na kisha funika na uache upikike kwa dakika 2 hivi.
Geuza ongeza chumvi kidogo na funika uchemke kwa muda wa dakika mbili hivi .
Mchicha upo tayari na unaweza kula na ugali, wali, ndizi nk

Rasilimali kwenye NUS
CONTACT SWISSAID Tanzania







